|
|
UONGOZI WA MNMA WARIDHISHWA NA USHIRIKI NA MCHANGO WA WANAWAKE KATIKA KUTIMIZA MAJUKUMU
Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Richard Kangalawe amesema ushiriki na mchango wa wa wanawake katika kutimiza majukumu na malengo ya Chuo upo kwa kiwango kikubwa na unaridhisha.
Akizungumza leo katika kongamano maalumu la kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Wanawake kwa niaba ya Mkuu wa Chuo, Prof. Kangalawe amesema maadhimisho ya siku ya wanawake duniani huongeza chachu katika mapambano kwa jinsia zote.
Prof. Kangalawe amesema Katika kutambua hilo Chuo kimetenga idara maalumu ambayo ni idara ya jin ...
ia inayozungumzia masuala ya kijisnia na kuhakikisha yanapewa Kipaumbele.
Amesema Chuo kimeona ni vyema kuandaa kongamano la Chuo kwa lengo la kutoa fursa kwa Wanawake kushiriki kwa pamoja, kwa lengo la kutafakari pamoja na kuona namna bora ya kutatua changamoto mbalimbali katika jamii.
Kwa upande wake Naibu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala Dkt. Evaristo Haulle amesema ni muda muafaka kwa Wanawake kujifakari na kuona namna bora ya kutatua changamoto zinazowakabili.
Naye Mratibu wa dawati la jinsia Dkt Patricia Mwesigwa amesema siku hii ina umuhimu katika kusherehekea siku ya Mwanamke duniani katika kupambania haki za msingi za Mwanamke.
Dkt. Mwesigwa amesema Katika kupambana na ukatili wa kijinsia Chuo kimeanzisha dawati maalumu la jinsia kwa lengo la kupokea na kushughulikia matatizo ya kijinsia, ukatili wa kijinsia, kubuni mfumo mzuri wa kutoa taarifa zinazohusu ukatili wa kijinsia, kufanya tathmini ya vitendo vya kijinsia katika jamii au taasisi husika.
Chimbuko la siku ya Mwanamke duniani ilianza Machi, 1975 lengo likiwa ni kuikunbusha dunia katika kuzungumzia haki za wanawake
Kauli mbiu ya Wananake kwa mwaka huu inasema Wanawake na Wasichana 2025: tuinarishe haki, usawa na Uwezeshaji.
Imeandaliwa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
6.03.2025
Read more >
[ 2025-03-12 ]
|
|
|
|