PROF. MAPESA AINISHA MAFANIKIO YA CHUO NDANI UONGOZI WA DKT SAMIA
Mkuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) Prof. Haruni Mapesa leo amekutana na Wahariri na Waandishi kwa lengo la kuzungumzia mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka Minne ya Uongozi wa Mhe. Raia Samia Suluhu Hassan madarakani. Prof.Mapesa ameyataja mafanikio 13 yaliyopatika ndani ya miaka minne ya uongozi wa awamu ya sita kuwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya chuo kwenye kampasi zote tatu za chuo hicho ambazo ni Kivukoni Dar es Salaam,Karume Unguja na Pujini Pemba. Amezungumza hayo leo katika Kampasi ya Kivukoni jijini D ... r es Salaam ambapo alisema Ujenzi wa Maktaba unaoendelea utakuwa na uwezo wa kutumiwa na wanafunzi 2,500 kwa wakati mmoja na kuwa mradi huo utagharimu kiasi Cha Sh. bilion 16 hadi kukamilika kwake na kwamba mpaka sasa tayari zaidi ya Sh bilioni tano zimelipwa " Pia ndani ya Kampasi ya Kivukoni kutakuwa na maboresho ya miundombinu ya kufundishia na kujifunzia ili kuongeza ubora wa mafunzo na kufunga vifaa mbalimbali Vya kufundishia katika kumbi za mihadhara,"alisema Prof Mapesa Alisema.katika Kampasi ya Karume iliyoko Unguja Zanzibar kazi ya ujenzi wa Mabweni yenye uwezo wa kulaza wanafunzi 1,536 inaendelea, mradi huo utagharimu kiasi Cha Sh bilioni 16 ambapo mpaka.sasa kiasi Cha Sh bilioni 5.8 zimeshatolewa Alisema kwa upande wa Kampasi ya Pemba iliyoko eneo la Pujini kazi ya ujenzi wa madarasa kumi imekamilika na yanatumika.kwa kujifunzia Aidha ujenzi wa jengo la utawala na ukumbi wa mihadhara unaendelea na kiasi Cha Sh bilioni 2.6 kimetengwa kwa ajili ya ujenzi huo Prof Mapesa aliyataja mafanikio mengine kuwa ni ongezeko la programu za mafunzo katika ngazi ya shahada ya umahiri kutoka programu sita mwaka 2014 hadi kufikia 53 mwaka huu wa 2025 Alisema chuo kimetenga bajeti ya Sh Milioni 100 kwa ajili ya kuwezesha wahadhiri kufanya tafiti mbalimbali zenye maslahi kwa chuo na taifa kwa ujumla " Pamoja na kiufanya utafiti chuo kimeendelea kufanya ushauri wa kitaalamu kwa Sekta ya umma na binafsi ikiwemo kutoa mafunzo ya muda mfupi," alisema Prof Mapesa Alisema chuo kinaendelea kutoa mafunzo ya Uongozi, Maadili na Utawala Bora kwa wadau wa Sekta ya Umma na Binafsi wakiwemo wanafunzi wote waliohitimu katika chuo hicho Alisema.kuhusu ongezeko la udahili wa wanafunzi katika Kampasi zote tatu umeongezeka kutoka wanafunzi 9521 mwaka 2019/20 Hadi kufikia wanafunzi 14,607 mwaka 2024/25 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 53.4 Hata hivyo alisema wahitinu katika Kampasi zote wameongezeka kutoka wahitinu 4,323 mwaka 2021 Hadi wahitinu 5,016 2024 sawa na ongezeko la asilimia 16 Akizungumza na Wahariri na Waandishi Prof.Mapesa amewataka Watanzania kutumia maktaba ya Chuo inayojulikana kwa jina la kibweta cha Mwalimu kusoma machapisho ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na tafiti zinazohusu falsafa zake ili kuyaishi maisha yake na kujenga taifa lenye amani weledi na uadilifu mkubwa. Pia amewataka kikitumia chuo hicho kwenye mafunzo ya muda mfupi katika taaluma za Read more >
[ 2025-03-20 ]
Visitors Counter
Flag Counter
Collaboration

TCU Link

NACTE Link
NECTA Link
ZHELB Link
HELSB Link
MoEST Link
MoEZ Link
Social Networks
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter
Contact us
Hotline : +255 (22) 2820041/47
P.O.BOX : 9193 Dar es Salaam,TANZANIA
Email : rector@mnma.ac.tz
Location : Kivukoni Dar-es-salaam