|
|
WAZIRI MKUU MSTAAFU MIZENGO PINDA ATEMBELEA BANDA LA MNMA
Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Mizengo Pinda leo ametembelea Banda la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere katika maonesho ya VETA yanayoendelea katika viwanja vilivyopo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam( JNICC).
Mhe. Mizengo Pinda amekipongeza Chuo kwa kushiriki maonesho hayo, ambapo amejionea bunifu mbalimbali za Wanafunzi wa Chuo na kusema kuwa anatambua mchango unaotolewa na Chuo hicho.
“Nakifahamu vizuri Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere,ambapo muasisi wake ni baba wa Taifa na kilianzish ...
a kwa lengo la kuwaandaa viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali”, alisema Mhe. Mizengo Pinda.
Mhe. Pinda alipongeza kazi mbalimbali alizojionea kutoka kwa wabunifu wa Chuo hicho na kuvutiwa na ubunifu wa mfumo wa namna kuandaa Kitalu cha mbegu za mpunga ( trans- plant cultivation alert system)
Maonesho hayo ya VETA yanafanyika ikiwa ni sehemu ya Taasisi hiyo kutimiza miaka 30,ambapo kesho tarehe 21 Maadhimisho yatafikia kilele.
Imeandaliwa na :
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
20.03.2025
Read more >
[ 2025-03-20 ]
|
|
|
|