PROF. MAPESA AWATAKA VIONGOZI WA WANAFUNZI KUSOMA KWA BIDII NA KUFAULU
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Haruni Mapesa jana tarehe 03.06.2025 amemwapisha Waziri Mkuu mpya wa Serikali ya Wanafunzi ya Chuo hicho (MASO) TItusy Mdasy. Akizungumza baada ya uapisho huo, Prof.Mapesa ameitaka serikali hiyo ya Wanafunzi kufanya kazi zao za uongozi kwa kuheshimiana na kushirikishina katika hatua mbalimbali za kutatua Changamoto. Prof.Mapesa amewaeleza viongozi hao kuwa wao ni daraja kati ya Uongozi wa Chuo na Wanafunzi wenzao ambao wanaowaongoza, hivyo lazima wawe mfano bora katika masuala mbalimbali. ... kuu huyo wa Chuo amewataka viongozi hao kusoma kwa bidii na kufanya vizuri katika mitihani yao ili wale wanaowaongoza waige. Prof. Mapesa amewataka pia viongozi hao kuheshimiana na Wafanyakazi huku akiwakumbusha kila kiongozi atimize majukumu yake kulingana na nafasi aliyoteuliwa nayo. " Kila mmoja akatimize majukumu yake kulingana na nafasi yake na si vinginevyo, isit9kee Waziri Mkuu akatamani nafasi ya Makamu wa Rais, au Waziri wa kawaida akatamani nafasi ya Waziri Mkuu, au Mbuge akatami nafasi ya Waziri, kila mmoja atumikie nafasi yake na sivinginevyo. Uapisho wa Waziri Mkuu huyo pia ulihudhuriwa na Naibu Mkuu wa Chuo anaesimamia Taaluma,Utafuti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Richard Kangalawe na Naibu Mkuu wa Chuo anaesimamia Mipango, Fedha na Utawala Dkt. Evaristo Haulle. Imetolewa na; Kitengo Cha Mawasiliano na Masoko CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE 04.06.2025 Read more >
[ 2025-06-04 ]
Visitors Counter
Flag Counter
Collaboration

TCU Link

NACTE Link
NECTA Link
ZHELB Link
HELSB Link
MoEST Link
MoEZ Link
Social Networks
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter
Contact us
Hotline : +255 (22) 2820041/47
P.O.BOX : 9193 Dar es Salaam,TANZANIA
Email : rector@mnma.ac.tz
Location : Kivukoni Dar-es-salaam