|
|
PROF.MAPESA AMTAKA MKANDARASI KUKAMILISHA MRADI ALIOPEWA KWA WAKATI
Mkuu wa Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Haruni Mapesa leo juni 04,2025 ameongoza kusaini mkataba wa ujenzi wa Jengo la Madarasa na Ofisi za walimu katika kampasi ya Kivukoni Dar es salaam.
Akizungumza baada ya kusaini Mktaba huo Prof.Mapesa amemtaka Mkandarasi wa kampuni ya Home Africa Investiment Corporation Limmited kuhakikisha anatimiza kazi kwa mujibu wa mkataba na si vinginevyo.
Prof. Mapesa amemtaka Mkandarasi kuelewa kwamba mradi huu ni wa serikali na utatumia fedha za umma hivyo amemtaka Mkandarasi kuujenga kwa kufuata vi ...
ango na ubora wa hali ya juu kwa kila kitu.
Vilevile amemtaka Mkandarasi akamilishe mradi kwa wakati uliopangwa ili kurahisisha matumizi yanayotarajiwa katika Majengo husika.
Kwa mujibu wa Mkuu wa kitengo cha Manunuzi Majanjara Semba ameeleza kuwa mpaka mradi huo utakapokamilika utakuwa umetumia Jumla ya fedha za kitanzania zaidi ya Shilingi Milioni 932, na kuwa mradi huo utakamilika baada ya miezi minne kuanzia mwezi wa 6 hadi mwezi wa 10, 2025.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Milki Mhandisi Mohamed Mrindoko alieleza kwamba Jengo hilo litakapokamilika
litakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 630, ofisi za wafanyakazi 14 zitakazotumiwa na Wafakazi 70.
Kwa mujibu wa
Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya Home Africa Investment Corporation Limmited Oliver Biseko ameishukuru MNMA kwa kuiamini kampuni hiyo baada ya kushinda Zabuni ambapo ameahidi kukamilisha kazi ikiwa katika ubora na katika muda uliopangwa.
Utiaji saini Mkataba huo pia ulishuhudiwa na Menejimenti ya Chuo.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
04.06.2025
Read more >
[ 2025-06-04 ]
|
|
|
|