|
|
KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU AKIPONGEZA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kimepongezwa kwa kushiriki vizuri katika kutoa mafunzo kwa vijana katika kupambana na rushwa, kupambana na dawa za kulevya, kujikinga na maambukizi ya virusi vya Ukimwi, namna ya kuwa Waadilifu na Wazalendo katika nchi yao.
Pongezi hizo kwa Chuo zimetolewa Leo na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 Ismail Ali Ussi wakati wa ziara ya Mwenge wa Uhuru katika Chuo hicho katika Kampasi ya Karume Zanzibar .
Akizungumza na vijana walioshiriki mafunzo hayo kutoka Wilaya ya Magharibi A pamoja na wa ...
afunzi wa Chuo hicho amewapongeza vijana kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mafunzo hayo pia amewasisitiza vijana kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi itakapofika wakati wa uchaguzi Mkuu oktoba mwaka huu.
Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 amesema kuwa Mwenge wa Uhuru unaonyesha mwanga ndani ya nchi na katika mipaka ya nchi, pia unaonyesha matumaini, upendo na ushindi hivyo kila kijana anapaswa kutambua umuhimu wa Mwenge wa Uhuru.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampasi wa Karume Dkt. Rose Mbwete alimshukuru kiongozi huyo wa mbio za Mwenge kwa kutambua mchango wa Chuo kwa Taifa.
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
21.06.2024
Read more >
[ 2025-06-22 ]
|
|
|
|