PROF. MAPESA AZINDUA BASI JIPYA LA CHUO
Mkuu wa Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Haruni Mapesa leo amezindua rasmi basi jipya la Chuo aina ya TATA MARCOPOLO.
Akizungumza na watumishi wakati akizindua basi hilo amesema hii ni hatua kubwa kwa taaaisi kuwa na chombo cha usafiri cha aina hii na kuwa kitarahisiaha shughuli za chuo kwa ufanisi.
Mapesa Amesema huu ni mwanzo na kuwa Chuo kitaendelea kuongeza vyombo vya usafiri zaidi kwa kuwa Taasisi nayo inakuwa.
Pia amewataka madereva kutunza vyombo hivyo ikiwa ni pamoja na kuzingatia Sheria za barabarani na kutoendesha ...
kwa mwendo wa haraka.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA NWALIMU NYERERE
25.06.2025
Read more >
[ 2025-06-27 ]