|
|
PROF. MAPESA AWATAKA WATUMISHI MNMA KUTOA HUDUMA BORA KWA WATEJA
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Haruni Mapesa siku ya Jumatano tarehe 23.07.2025 aliongoza Mkutano wa 12 wa baraza la Wafanyakazi ambapo amewataka watumishi wote kushirikiana katika kukitangaza Chuo.
Prof. Mapesa ameyasema hayo wakati wa Mkutano huo wa baraza uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Tamisemi- Kivukoni Feri, jijini Dar es Salaam.
" Jukumu la kukitangaza Chuo ni letu sote, kwa kuwa sisi wote tunafanya kazi hapa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, hivyo tushirikiane kwa pamoja na tuwe mabalozi katika ku ...
neza mengi mazuri yanayopatikana katika Chuo hiki."Alisisitiza Prof. Mapesa.
Mkuu huyo wa Taaaisi pia amewataka Watumishi kuhakikisha kila mmoja anatoa huduma nzuri na kwa wakati ili kuhakikisha malengo ya Taasisi yanafikiwa.
Kikao hicho cha siku moja pia kilijadili taarifa utekelezaji wa bajeti ya Chuo kwa mwaka wa fedha 2024/2025, pamoja na kutolea ufafanuzi hoja mbalimbali za Wafanyakazi .
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
24.07.2025
Read more >
[ 2025-07-26 ]
|
|
|
|