|
|
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE NA KAMANDI YA JESHI LA WANAMAJI KUENDELEA KUDUMISHA USHIRIKIANO
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) Prof. Haruni Mapesa amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Wanamaji (Navy Command) Meja Jenerali Ameir Hassan ambapo lengo la mazungumzo hayo ni kuendeleza ushirikiano kujitambulisha, na kuendeleza kudumisha mahusiano mema baina ya Taasisi hizo mbili.
Mazungumzo ya viongozi hao yalifanyika jana Agosti 11, 2025 katika ukumbi wa Generation uliopo katika Kamandi ya Jeshi la Wanamaji jijini Dar es salaam, ambapo Taasisi hizo ni majirani .
Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la ...
Wanamaji, Meja Jenerali Ameir Hassan amesema jeshi hilo litaendela kutoa ushirikiano kwa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kama ambavyo siku zote wamendelea kutoa hasa katika eneo la ulinzi.
Akielezea historia fupi ya Kamandi ya Jeshi la wanamaji kwa niaba ya Mkuu wa Kamandi hiyo, Luteni Kanali Fatma Mnekano alisema Kamandi ya Jeshi la wanamaji ilianzishwa Desemba 06, 1971 kwa ushirikiano wa kindugu kati ya Tanzania na Jamhuri ya watu wa China na kupandishwa hadhi kuwa Kamandi ya Jeshi la wanamaji tareheJuni 01 1981.
Luteni kanali Mnekano alibainisha majukumu ya kamandi hiyo ya jeshi kuwa ni pamoja na Kulinda mipaka ya baharini na maziwa makuu, kudhibiti kikamilifu ulinzi wa Pwani ya Tanzania, Ulinzi wa Bahari ya Tanzania na yote yaliyomo na kuhakikisha vikosi vilivyo chini ya kamandi hiyo vina ulinzi wa kutosha wa nchi kavu, anga na majini na kufanya utafiti wa mambo ya ulinzi wa pwani.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Haruni Mapesa amemshukuru Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la wanamaji kwa kumkaribisha na kufanya mazungumzo ya pamoja ya kuendeleza kudumisha ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili hasa katika huduma za ulinzi pamoja na huduma za hospitali zinazotolewa katika Kamandi ya Jeshi hilo.
“Chuo kitaendelea kushirikiana na Kamandi ya Jeshi la wanamaji hasa katika maeneo yanayotuzunguka na tunashukuru sana kwa kuendelea kuwapokea vijana wetu katika Kituo chenu cha afya, tutaendelea kushikiriana kadri ya uwezo wetu na hata uwepo wenu unawafanya wanafunzi wetu wanasoma kwa utulivu kwa sababu wanajua tumepakana na jeshi’’, alisema Prof. Mapesa.
Naye, Naibu Mkuu wa Chuo anayesimamia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa kitaalamu Prof. Richard Kangalawe alielezea historia na chimbuko la Chuo cha Kivukoni ambacho kilianzishwa rasmi tarehe 29 Julai 1961, na kilianzishwa kutokana na Mkutano Mkuu wa chama cha TANU wa Tabora mwaka 1958 na Hayati Mwl. Nyerere ndiye aliyekuwa mwanzilishi wa chuo na kwa kipindi hicho kiliitwa Chuo cha Kivukoni, Haja ya kitaifa ya upanuzi wa elimu ya juu ilipelekea Chuo cha Kivukoni kugeuzwa kuwa taasisi ya elimu ya juu mwaka 2005, na kusababisha kuanzishwa kwa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere. Kwa sasa Chuo kina Kampasi tatu, Kampasi ya Kivukoni iliyopo Kivukoni - Dar es Salaam, Kampasi ya Karume iliyopo Unguja - Zanzibar na Kampasi ya Pemba iliyopo Wilaya Chakechake Pemba.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Masok
Read more >
[ 2025-08-12 ]
|
|
|
|