PROF. MAPESA AISHUKURU TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI KWA KUKIAMINI CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE.
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Haruni Mapesa leo amekutana na kufanya mazungumzo na timu ya Wafanyakazi wa Chuo ambao wamechaguliwa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya Kutoa Elimu ya mpiga Kura wa Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani kwa mwaka 2025. Akizungumza na timu hiyo maalumu iliyochaguliwa kushiriki zoezi hilo katika kikao cha pamoja cha Ufunguzi wa Programu ya Kutoa Elimu ya Mpiga Kura katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 Prof. Mapesa ameishukuru Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa kukiamini Chuo hicho ... ushiriki zoezi hilo muhimu ambapo amewataka washiriki wa zoezi hilo kusoma masharti na kuzingatia maelekezo yote yaliyotolewa na Tume kwa ajili ya zoezi hilo ili kuhakikisha kazi inafanyika kwa weledi na uelewa mkubwa. Profesa Mapesa amesema zoezi la kutoa Elimu ya Mpiga kura ni suala muhimu kwa mustakabali wa Taifa , hivyo amewataka washiriki wote kuhakikisha wanakuwa na uwelewa wa pamoja na kuwa na mtizamo unaofanana kwa lengo la kuwa na Umoja, upendo na Amani katika Taifa. Naye Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na ushauri wa Kitaalamu Prof. Richard Kangalawe amesema kuwa nafasi hii ni nzuri kwa kuwa huduma inaenda kutolewa kwa Wananchi na pia ni sehemu sahihi ya kusaidia kukitangaza Chuo kwa wadau mbalimbali hapa nchini. Kwa upande wake Naibu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala Dkt. Evaristo Haulle amesema jukumu kubwa la Chuo ni Kutoa mafunzo katika ngazi mbalimbali, kufanya Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu lakini katika hili la kutoa Elimu kwa Mpiga kura ni huduma ya moja kwa moja ambayo wananchi wanaenda kuipata kupitia Chuo hicho. Kupitia kikao hicho washiriki walipokea ripoti fupi ya programu na mwongozo wa Elimu ya Mpiga Kura, Sheria na makosa ya Uchaguzi ambapo bajeti na mpango kazi wa namna zoezi hilo litakavyofanyika viliwasilishwa. Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Masoko CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE 15.09.2025 Read more >
[ 2025-10-01 ]
Visitors Counter
Flag Counter
Collaboration

TCU Link

NACTE Link
NECTA Link
ZHELB Link
HELSB Link
MoEST Link
MoEZ Link
Social Networks
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter
Contact us
Hotline : +255 (22) 2820041/47
P.O.BOX : 9193 Dar es Salaam,TANZANIA
Email : rector@mnma.ac.tz
Location : Kivukoni Dar-es-salaam