PROF. MAPESA AZINDUA MRADI WA MILIONI 200 UNAOFADHILIWA NA COSTECH
Mkuu wa Chuo cha Kumbumbu ya Mwalimu Nyerere Prof Haruni Mapesa leo amezindua mradi wa utafiti wenye thamani ya kiasi cha shilingi Milioni 200 unaohusu matumizi ya Akilimnemba na taarifa za kisatelaiti katika kutatua athari za mabadiliko ya tabia nchi kwenye uzalishaji endeleevu wa Chakula (FOCUS). Uzinduzi wa mradi huo umefanyika katika kampasi ya Kivukoni ya Chuo hicho jijini Dar es Salaam ambapo Prof. Mapesa amewapongeza walioshinda mradi huo unaotarajiwa kukamilika baada ya miaka mitatu. Prof. Mapesa amewataka watafiti wanaoshiriki mr ... di huo kuzingatia wajibu wao katika kukamilisha mradi kwa wakati huku ukiwa na matokeo mazuri ikizingatiwa kuwa fedha zinazotumika ni za serikali hivyo lazima wakiwakilishe Chuo vizuri. Amewataka watafiti kufanya kazi kwa ushirikiano na umoja, na kuwa kazi hiyo ikikamilika kwa mafanikio makubwa na katika muda ulipangwa maana kwa kufanya hivyo litakuwa ni jambo jema ambalo litasaidia kufungua mianya ya kuendelea kupata ufadhili zaidi. “Watafiti wa mradi huu, Suala siyo kupata fedha suala ni mradi ulete matokeo,kumbukeni fedha hizi ni za Serikali na zinasimamiwa na wataalamu wa fedha hivyo fedha hizi zikatumike Kama inavyotakiwa, nendeni mkafanye kazi kwa uwajibikaji, mkawe wamoja na ushirikiano huku mkizingatia kuwa fedha hizi ni za serikali na zitakaguliwa kuonesha namna zilivyotumika,”alisisitiza Profesa Mapesa. Naye Naibu Mkuu wa Chuo anaesimamia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Richard Kangalawe amewakumbusha watafiti kuhakikisha mradi huo unashirikisha Wataalamu kutoka katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha mradi huo unafanikiwa. Naye mtafiti Mkuu wa mradi huo Dkt. Sifuni Lusiri ameeleza kuwa Mabadiliko ya Tabia nchi yanaathiri maeneo mbalimbali kwa namna tofauti tofauti hivyo maeneo yalichaguliwa kwa ajili ya utafiti yanawakilisha maeneo ya nchi yanayopata kiasi kikubwa cha mvua Iringa (Kilolo) ambayo ni nyanda za juu kusini, na eneo lingine ni Dodoma (Kondoa ) kanda ya Kati inawakilisha maeneo yanayopata mvua kidogo. Mradi huo wa Utafiti unafadhiliwa na Tume ya Taifa ya Sayasni na Teknolojia (COSTECH) na msimamizi wake Mkuu ni Dkt. Sifuni Lusiru ambaye ni Mkurugenzi wa idara ya Utafiti na ushauri wa Kitaalamu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere akishirikiana na watafiti wengine ambao ni Dkt. Asnath Malekela (MNMA), Prof. Richard Kangalawe (MNMA), Dkt Olipa Simon ( UDSM), Dkt. Evaristo Haulle (MNMA) na Theopister Kilawa (MNMA). Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano na Masoko Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere 30.09.2025 Read more >
[ 2025-10-01 ]
Visitors Counter
Flag Counter
Collaboration

TCU Link

NACTE Link
NECTA Link
ZHELB Link
HELSB Link
MoEST Link
MoEZ Link
Social Networks
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter
Contact us
Hotline : +255 (22) 2820041/47
P.O.BOX : 9193 Dar es Salaam,TANZANIA
Email : rector@mnma.ac.tz
Location : Kivukoni Dar-es-salaam