|
|
|
MNMA YAMUENZI MWL. J.K NYERERE KATIKA KUHAMASISHA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), imeadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 36 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu J.K Nyerere katika kuhamasisha matumizi ya Teknolojia katika Elimu, Habari na Maendeleo ya watu.
Akizungumza wakati wa kufungua kongamano la Nne la Kitaaluma la Kumuenzi Mwalimu J.K Nyerere Profesa Mapesa amebainisha kuwa Umoja, Mshikamano wa watu kwa kutumia Teknolojia vinatakiwa kuenziwa sana ili kuimarisha maono na falsafa za Baba wa Taifa.
Kongamano hilo lilifanyika katika kampasi ya Kivukoni ya Chuo hicho lilik ...
wa na mada kuu isemayo Maono ya Mwalimu Nyerere kuhusu Sayansi na Teknolojia kwa Maendeleo Endelevu.
Prof. Mapesa amesema MNMA imeiweka Teknolojia kuwa ni kiiini cha kuendeleza falsafa za Mwalimu kwa kila mtanzania aweze kupata elimu bila kujali yupo eneo gani, kila mtanzania aweze kupata mawaidha ya Mwalimu yanahohusu umoja na mshikamano kwa kutumia teknolojia.
Prof. Mapesa amesema Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kimejipanga katika upande wa Elimu kuhakikisha kinatumia zana za kisasa katika suala la ufundishaji wa wanafunzi na kuwafikia wadau wengi hasa katika uwekezaji wa akili mnemba ili kurahisisha utendaji kazi wa wafanyakazi wa MNMA.
Kwa upande wake, Naibu Mkuu wa Chuo Profesa Richard Kangalawe anayesimamia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalaam amesema kitabu kilichozinduliwa leo ni zao la kongamano lililofanyika mwaka jana lililobeba mada iliyohusu Falsafa za Mwalimu Kuhusu Uongozi na Maendeleo Endelevu.
"Mawasilisho yaliyopo kwenye kitabu hiki ni matokeo ya utafiti na makongamano, hii ni njia mojawapo ambapo kama taasisi ya Elimu ya juu tuna majukumu makubwa matatu ikiwemo kufundisha, kuandaa vijana kwa kuwapa mafunzo mbalimbali darasani kwa vitendo, pili ni kuwapa maarifa na kufanya utafiti kwa lengo la kupata majibu yenye changamoto mbalimbali zinazoukabili jamii’’, alisema Prof. Kangalawe.
Prof. Kangalawe ameongeza kuwa kitabu hicho kinatoa mtazamo wa ujumla kuhusu masuala ya uongozi na jinsi uongozi unavyoweza kupelekea maendeleo endelevu ya kijamii, kiuchumi na kisiasa katika ulimwengu wa sasa pia na kwa namna gani ambavyo uongozi thabiti unavyoweza kupelekea maendelo endelevu katika taifa letu.
Imeandaliwa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
17.10.2025
Read more >
[ 2025-10-18 ]
|
|
|
|