|
|
|
MAHAFALI YA MNMA-KAMPASI YA KARUME YAFANA WAHITIMU 1,249 WATUNUKIWA VYETI.
Wanafunzi 1,249 wamehitimu kozi mbalimbali katika Mahafali iliyofanyika leo katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kampasi ya Karume- Zanzibar.
Akizungumza wakati wa Mahafali hayo ya 10 ya Kampasi hiyo Mwenyekiti wa bodi Mhe. Stephen Wasira amewapongeza wahitimu na kuwataka wasibweteke na kiwango cha Elimu walichokipata, na badala yake wajiendeleze ili kulitumikia Taifa.
Mzee Wasira amewakumbusha Wahitimu kuwa Nchi hii ni yetu sote, ili nchi iendelee Suala la Amani ni la lazima, hivyo vijana wa Tanzania msikubali kutumika na taaais ...
ambazo zinataka kuondoa Amani, msikubali hilo.
Kiongozi huyo amewataka Wanafunzi hao kuwa Wazalendo katika nchi yao, na wasikibali kudanganyika.
Hatuna ugomvi na nchi yeyote lakini wapo ambao hawapendi tuendelee, wanataka tuendelee kuwa ombaomba.
Mwenyekiti wa bodi ameipongeza Menejimenti ya bodi na Wafanyakazi wote kwa kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza malengo ya Taasisi iliyojiwekea.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Prof. Haruni Mapesa amesema Chuo kinaendelea kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia ili kuhakikisha Maarifa na ujuzi vinavyotolewa Chuoni vinakuwa ni vyenye manufaa.
Read more >
[ 2025-12-01 ]
|
|
|
|