|
|
|
KONGAMANO LA WAHITIMU LAFANYIKA MNMA PROF. MAPESA AAHIDI MAKUBWA
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Prof. Haruni J. Mapesa amewaahidi viongozi wa Kusanyiko la Baraza la Wahitimu kuwa kuanzia kusanyiko lijalo kutakuwa na mtu mahususi atakayeshughulikia masuala ya kusanyiko la baraza la Wahitimu katika chuo.
Mkuu wa chuo ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza na Kusanyiko la baraza la Wahitimu (Convocation) lililofanyika katika ukumbi wa Utamaduni katika kampasi ya Kivukoni.
Prof. Mapesa amesema kuanzia kusanyiko lijalo baraza litakuwa na mtu maalumu atakayeshughulikia masuala ...
ya kusanyiko la baraza la wahitimu kama ambavyo hotuba ya viongozi wa baraza la Wahitimu ilivyoomba.
"Nawaahidi kuzifanyia kazi changamoto zilizoanishwa na baraz Baraza la Wahitimu kwa kuliwezesha kuwa na mratibu atakayesimamia shughuli zote ili baraza liweze kufanya kazi kwa weledi", alisema Prof. Mapesa.
Mkuu huyo wa taasisi alisema Chuo kinatarajia kuanzisha Shahada za Uzamivu (PhD), za viwango vya kimataifa ili kuwezesha taifa kuwa na wataalamu wa kutosha.
Kupitia kongamano hilo la Wahitimu Prof . Mapesa ametumia nafasi hiyo kuwapongeza wanafunzi waliohitimu na kuwakaribisha wanafunzi wote wapya waliojiunga na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na amewahidi chuo kitawapatia Elimu bora na inayoendana na Teknolojia..
Kwa upande wake Katibu wa baraza la Wahitimu Jumanne Muruga amesema kongamano hilo linatoa fursa kwa wadau mbalimbali na kuwapa nafasi ya kutoa mawazo yao katika mada mbalimbali zinazowasilishwa kupitia kongamano hilo..
Akitoa salamu za shukrani Mwenyekiti wa Kusanyiko la wahitimu Gerald Mwamsiku amewaasa wahitimu kutojiingiza katika makundi ambayo si rafiki yanayoweza kuwaharibia ndoto zao ambazo wamejipangia katika kutimiza malengo yao na Taifa kwa ujumla.
Wanafunzi waliofanya vizuri katika upande wa taaluma na Uongozi wa Serikali ya Wanafunzi ( MASO) walitunukiwa vyeti.
Mada iliyowasilishwa katika kongamano hilo ni *Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kinavyojipambanua Katika Kuchagiza Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa Vijana ambayo
iliwasilishwa na Dkt. Ahmed Sovu Mhadhri wa Chuo hicho.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
27.11.2024
Read more >
[ 2025-12-03 ]
|
|
|
|