PROF MAPESA AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI MNMA, ATAKA UBUNIFU ILI KUONGEZA MAPATO YA CHUO
PROF MAPESA AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI MNMA, ATAKA UBUNIFU ILI KUONGEZA MAPATO YA CHUO Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Haruni Mapesa mwishoni mwa wiki Januari 30, 2026 aliendesha kikao cha kuzindua baraza jipya la Wafanyakazi na kuendesha Mkutano wa 13 wa baraza hilo uliofanyika kwenye ukumbi wa Chuo Chuo cha Utumishi wa Umma, (TPSC) jijini Dar es salaam. Kupitia kikao hicho Prof. Mapesa ameendelea kuwahimiza Watumishi kuendelea kuwa wabunifu katika nyanja mbalimbali zitakazoiingizia Taasisi mapato, ikiwe ... o kuongeza kozi ambazo zinatawavutia vijana katika kujiajiri. Kabla ya kikao kuendelea, Mwenyekiti wa baraza hilo Prof. Mapesa aliwaongoza Wajumbe wa baraza kufanya uchaguzi wa Katibu na Katibu Msaidizi ambapo majina mawili yaliyopendekezwa na Menejimenti ya Chuo yaliwasilishwa na kisha wajumbe wa baraza walipiga kura kuchagua viongozi hao. Jumla ya wajumbe 45 wa baraza waliopiga kura Kati yao wajumbe 27 walimpa kura ya ndiyo Yohana Cleopa, (Katibu) na wajumbe 18 walimpa kura ndiyo Jovita Rwezaulaya (Katibu Msaidizi) Pia kikao hicho cha baraza la Wafanyakazi kilipitia maoteo ya bajeti ya Chuo kwa mwaka wa fedha 2026/2027 na kutoa maoni na kushauri kwa lengo la kuongezea Chuo Mapato. Baraza hilo pia lilipitia Sera ya Jinsia, wajumbe wa baraza waliwasilisha hoja mbalimbali ambazo Menejimenti ilitolea majibu ya hoja hizo. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na viongozi wa vyama vya Wafanyakazi ikiwemo Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Ufundi Stadi, Ushauri, Habari na Utafiti-RAAWU -na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu-THTU -ngazi ya Taifa . Read more >
[ 2026-02-26 ]
Visitors Counter
Flag Counter
Collaboration

TCU Link

NACTE Link
NECTA Link
ZHELB Link
HELSB Link
MoEST Link
MoEZ Link
Social Networks
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter
Contact us
Hotline : +255 (22) 2820041/47
P.O.BOX : 9193 Dar es Salaam,TANZANIA
Email : rector@mnma.ac.tz
Location : Kivukoni Dar-es-salaam
W
E
L
C
O
M
E