|
|
|
PROF. MAPESA AAHIDI KUIMARISHA MAZINGIRA YA KAZI NA KUBORESHA MOTISHA ZA WATUMISHI.
PROF. MAPESA AAHIDI KUIMARISHA MAZINGIRA YA KAZI NA KUBORESHA MOTISHA ZA WATUMISHI.
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Prof. Haruni Mapesa, amefanya kikao jana februari 3,2026 na Watumishi na Wanafunzi waliopo Kampasi ya Pemba, na kueleza kuwa Mafanikio yanayoshuhudiwa hivi sasa katika kampasi hiyo ni matokeo ya Umoja, Weledi, na Ari ya juu miongoni mwa Wafanyakazi, jambo ambalo limeendelea kukijengea chuo heshima kubwa.
Profesa Mapesa amewaeleza Watumishi kuwa Mpango Mkakati mpya wa Miaka Mitano wa kuanzia 2025/2026 – 20 ...
0/2031 vipaumbele vitakavyoongoza chuo katika kipindi cha miaka mitano ijayo vitafanya chuo kuwa kitovu cha ushindani zaidi ikiwemo kuongeza Udahili wa Wanafunzi sambamba na kuboresha Miundombinu ya kujifunzia, kuboresha Mitaala na kuongeza Programu mpya zenye ushindani, Lengo likiwa ni kuzalisha wahitimu wenye Ujuzi wa kisasa watakaotatua changamoto katika Jamii.
Katika hatua nyingine, Prof. Mapesa alisisitiza kuwa chuo kimejipanga kuimarisha Mazingira ya kazi, ikiwa ni pamoja na kupitia upya stahiki mbalimbali za Wafanyakazi na kuimarisha mifumo ya motisha, ili kuhakikisha mtumishi wa MNMA anafanya kazi katika hali ya Amani, Utulivu, na Weledi wa hali ya juu.
Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Taasisi Prof. Mapesa alizungumza na Wanafunzi na kuwaeleza kuwa wamefanya Chaguo sahihi kujiunga na MNMA kwa kuwa ni kioo cha masuala ya Uongozi na Maadili.
Prof. Mapesa amewataka Wanafunzi kutambua thamani ya Chuo ikiwa ni pamoja na kujivunia kuwa sehemu ya familia ya MNMA maana kwa Miongo kadhaa Chuo kimekuwa kikitoa mafunzo kwa Viongozi na Wataalamu wenye Weledi na Uzalendo,
hivyo amewataka Wanafunzi kujiepusha na matendo yote maovu yanayoweza kukatisha ndoto zao za kimasomo na malengo yao kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampasi ya Pemba Dkt. Ernest Haonga amemshukuru na Kumpongeza kwa dhati Mkuu wa Chuo Prof. Mapesa kwa mageuzi na kazi mzuri anayoifanya, ambapo kwa sasa Kampasi ya Pemba imepata sura mpya na Mazingira bora ya utendaji kazi, jambo ambalo limekuwa chachu ya mafanikio na utulivu kwa watumishi na wanafunzi wa kampasi hiyo.
Read more >
[ 2026-02-26 ]
|
|
|
|