|
|
|
PROF. MAPESA AINISHA MAFANIKIO YA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
PROF. MAPESA AINISHA MAFANIKIO YA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Prof. Haruni Mapesa Jana Machi 16, 2025 amekutana na kuzungumza na Wahariri na Waandishi kwa lengo la kuelezea mafanikio ya Chuo hicho ndani ya kipindi cha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Profesa Mapesa amesema, Chuo kimeshuhudia ongezeko la Wanafunzi waliodahiliwa ambapo idadi imepanda kutoka wanafunzi 14,627 mwaka 2024/25 hadi kufikia 15,745 mwaka 2025/26 ongezek ...
hilo linajumuisha kampasi za Kivukoni, Karume – Zanzibar, na Pemba, ongezeko hilo ni ishara kuwa jamii imejenga imani na Chuo.
Mkuu huyo wa Taasisi ameeleza kuwa katika kuimarisha ufanisi katika utendaji chuo kimeanza kutumia mfumo mpya wa utunzaji wa Kumbukumbu za kitaaluma ARMS (Academic Records Management System) unaosimamia Udahili, Mitihani, na malipo mbalimbali ya fedha Fedha kwa usalama, ikiwemo uboreshaji wa sheria na taratibu za Mitihani ili kuzalisha wataalamu wenye Maadili na kuongeza uadilifu wa matokeo na uwajibikaji miongoni mwa watumishi na wanafunzi.
Profesa Mapesa Pia amezungumzia Mradi wa ujenzi wa jengo la Maktaba itakayo kuwa na uwezo wa kutumiwa na wanafunzi 2,500 kwa wakati mmoja, ambalo pia litakuwa na Ukumbi wa Mihadhara wenye uwezo wa kutumiwa na wanafunzi 1,000 kwa wakati mmoja, unaendelea vizuri. Tayari fedha za kitanzania zipatazo shilingi billioni 6 zimeshatumika katika mradi huu unaotegemewa kutumia jumla ya shilingi Bilioni 16 hadi kukamilika kwake.
Profesa Mapesa amewaeleza Wahariri na Waandishi kuwa Chuo kimeajiri watumishi 88 (wanataaluma 23 na waendeshaji 65) ambapo Ajira mpya 57 na ajira za uhamisho 31. Ajira hizi zimepunguza changamoto ya uhaba wa watumishi, Kwa sasa Chuo kinaendelea na mchakato wa kuajiri watumishi wengine 69 kwa mujibu wa kibali cha Ajira mpya.
Read more >
[ 2026-03-18 ]
|
|
|
|