|
|
|
PROFESA MAPESA AZINDUA MBAO JANJA (SMART BOARD) KUENDANA NA TEKNOLOJIA
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Haruni Mapesa leo amezindua Mbao janja (Smart board) zinazotumika kwa ajili ya kufundishia ambapo amesema kutokana na Mabadiliko ya Kielektroniki matumizi ya vifaa kama Smart board ni lazima ili kuendana na Sayansi na Teknolojia.
Prof. Mapesa amesema ni lazima wanataaluma wakubaliane na Mabadiliko ya kiteknolojia katika matumizi ya kufundishia, kuelekeza na kujifunzia na kuwa kila mmoja awe sehemu ya mpango huo na kuwa kuwepo kwa mbao janja hizo kutasaidia kuendesha Semina na kufanyika ...
wa Mihadhara kwa wadau wengi kwa wakati mmoja bila kujali umbali.
Mkuu huyo wa Taasisi amewapongeza Wanataaluma kwa utekelezaji wa Majukumu yao ikiwemo uvumilivu, na kusema kuwa kazi ya kufundisha ni wito na ina wajibu mkubwa, hivyo Mbao Janja hizo 21 zitasaidia Chuo kuendana na Teknolojia
Akizungumza kabla ya Kumkaribisha Mkuu wa Taasisi, Naibu Mkuu wa Chuo anaesimamia Taaluma, Utafiti na ushauri wa Kitaaluma Prof.Richard Kangalawe amepongeza bodi ya Chuo kwa kuridhia kununuliwa kwa Mbao Janja hizo, huku akiwaomba Wanataaluma kutumia vifaa hivyo kwa usahihi, na endapo mtumiaji atapata changamoto basi ni vyema aombe msaada ili aeleweshwe.
Naye Naibu Mkuu wa Chuo anaesimamia Mipango, Fedha na Utawala Profesa Evaristo Haulle amesema uzinduzi wa Mbao janja hizo ni mkakati wa kuboresha Miundombinu ya ujifunzaji na ufundishaji, hivyo ameshauri kuwa mbao hizo zitumike kwa ufanisi.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
30.03.2026
Read more >
[ 2026-04-01 ]
|
|
|
|