|
|
|
PROF. MAPESA: CHAPISHENI TAFITI KWENYE MAJARIDA YANAYOTAMBULIKA
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Prof. Haruni Mapesa amewataka wanataaluma kuacha tabia ya kuchapisha makala zao kwenye Majarida yasiyotambulika ili kuzuia upotezaji wa nguvu na rasilimali za uchapishaji wa Tafiti.
Prof. Mapesa ameyasema hayo wakati akifungua Semina ya Uwasilishaji wa Makala Mijadala za a Kitaaluma iliyoandaliwa na Idara ya Lugha na Fasihii Chuoni hapo hafla iliyofanyika katika Kampasi ya Kivukoni jijini Dar es salaam.
Mkuu huyo wa Chuo amesema kuwa sasa Tasisi ipo katika hatua za ukuaji ikiwemo kuid ...
inishwa kwa Kitivo cha Uchumi na Biashara, ambapo chuo kimetenga kiasi cha shilingi milioni 120 kwa ajili ya tafiti na kuna mpango wa kuongeza fedha hizo ili kuwekeza zaidi kwa wahadhiri watakaofanya tafiti mbalimbali.
Naibu Mkuu wa Chuo anayesimamia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaaluma Prof. Richard Kangalawe amekipongeza Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii kupitia Idara ya Lugha na Fasihi kwa kuandaa semina hiyo na kuwahimiza washiriki kutumia fursa hiyo kuimarisha mawazo ya kitafiti, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha tafiti zote zinasajiliwa rasmi na machapisho yawe yenye ubora wa hali.
Kwa upande wake, Naibu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala Prof. Evaristo Haulle amewataka Wanataaluma kubadilika na kuanza kufikiria namna ya kuchangia asilimia 30 ya mapato ya ndani kupitia Tafiti na Miradi wanayoifanya badala ya kutegemea rasilimali na fedha za ndani za chuo pekee.
Akiwasilisha taarifa ya Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii, Mtiva wa Kitivo hicho Dkt. Luzabeth Kitali ameishukuru Menejimenti ya Chuo kwa Maelekezo na Ushauri na kuahidi kuwa idara yake imejipanga kikamilifu kusimamia ubora wa Tafiti, kuendeleza Uandishi ikiwa ni pamoja na kushiriki katika makongamano ya kitaaluma.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
21.05.2026
Read more >
[ 2026-05-22 ]
|
|
|
|