|
|
|
PROF. MAPESA AWATUNUKU VYETI WAELIMISHA RIKA NA AMEWATAKA KUZINGATIA NIDHAMU
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Haruni Mapesa amewataka Waelimisha rika ambao ni wanafunzi kuendelea kutumia na kuyaishi Maarifa waliyoyapata kwa kuwafundisha vijana wenzao wengine ili hekima yao ionekane katika jamii wanazoishi.
Prof. Mapesa amewaasa Wanafunzi hao kubadilika baada ya kupata mafunzo ya namna bora ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Ukwimi, Afya ya uzazi, kuacha kujiingiza kwenye makundi yasiyofaa, kujitambua na kuisha maisha yanayozingatia Maadili, Nidhamu na kuacha yale yote ambayo hayapendezi k ...
tika jamii.
Mkuu huyo wa Taasisi amewataka Waelimisha rika hao kuwa kielelezo katika jamii na kuwa elimu hiyo iwafae wakiwa hapa Chuoni na hata watakapotoka nje ya Chuo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Waelimisha Rika kwa niaba ya Wanafunzi wenzake Faidhu Maulid ameshukuru Uongozi wa Chuo kwa kuwezesha kujifunza kwa ufasaha na kuwa wanaahdi kwenda kutekeleza kama walivyofundishwa.
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
22.05.2026
Read more >
[ 2026-05-22 ]
|
|
|
|