|
|
|
PROF. MAPESA AWAPONGEZA WANAFUNZI WALIOSHIRIKI MICHEZO NA AAHIDI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA MICHEZO.
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Haruni Mapesa ameahidi kushughulikia changamoto mbalimbali za kimichezo ikiwa ni pamoja na kuboresha Miundombinu ya Michezo, kununua vifaa mbalimbali vya kimichezo vinavyohitajika ili Michezo iwe na tija Chuoni hapo.
Prof. Mapesa amesema hayo wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza Wanafunzi walioshiriki shirikisho la Michezo la Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (SHIMIVUTA) yaliyofanyika mwaka jana mkoani Tabora, ambapo Wanafunzi waliofanya vizuri walikabidhiwa fedha kama sehemu ya motisha na kut ...
kiwa kufanya vizuri Zaidi.
Katika Mashindano hayo ya SHIMIVUTA Chuo kiliibuka mshindi wa kwanza katika mbio za magunia mita 100 na kufanikiwa kupata Kombe, pia Chuo kilipata kikombe cha ushindi wa ufungaji bora katika mchezo wa kikapu pamoja na Cheti cha ushiriki.
Mkuu huyo wa Taasisi alisisitiza kuwa Michezo inafaida nyingi sana ikiwemo kuleta Furaha, Ajira, na Afya, hivyo aliwataka vijana kuhakikisha wanajitokeza kushiriki michezo mbalimbali inayochezwa Chuoni hapa.
Alisema kupitia Ushiriki wa Michezo hiyo ya SHIMIVUTA Chuo kinapata nafasi ya kujitangaza kwa Wadau mbalimbali.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
22.05.2026
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
Read more >
[ 2026-06-02 ]
|
|
|
|