PROFESA MAPESA AMEITAKA SERIKALI YA WANAFUNZI KAMPASI YA KARUME KUWA NA UMOJA NA NIDHAMU
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Haruni Mapesa jana ijumaa tarehe 29.05.2026 aliwaapisha Rais na Makamu wa Rais watakaoongoza Serikali ya Wanafunzi kwa Kampasi ya Karume Kwa mwaka wa 2026/2027. Walioapishwa kuongoza kwa nafasi ya Rais ni Yahya Abdalla Rashid na kwa upande wa Makamu wa Rais ni Rukia Suleiman Hakim. Katika hafla hiyo fupi, Profesa Mapesa aliwapongeza Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi waliomaliza muda wao kwa kutumikia vyema nafasi zao kwa Juhudi, Nidhamu na Utii. Profesa Mapesa amewataka viongozi w ... pya kuyaenzi yaliyo mema na kujifunza kutoka katika changamoto za watangulizi wao akisisitiza kuendelea kuboresha Umoja, Upendo miongoni mwao ikiwa ni pamoja na kushirikiana na Menejimenti ya Chuo kwa lengo la kufikia Malengo ya Taaaisi. Mkuu huyo wa Taasisi amesisitiza suala la kuendelea na Program za kukutana na jamii, kuendelea kukutana na kujadili masuala mbalimbali kwa Mujibu wa Sheria na Taratibu zinavyoelekeza. Kwa Upande wake Naibu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala Profesa Evaristo Haulle amewataka wanafunzi kutambua kuwa suala la Uchaguzi na Uongozi Kwa wanafunzi ni sehemu ya Elimu Kwa vitendo kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu, hivyo wanapaswa kuuchukulia uongozi kama fursa muhimu ya kuonesha namna watakavyokuwa imara kuziongoza jamii zinazowazunguka. Naye Mkurugenzi wa Kampasi ya Karume - Zanzibar Dkt. Sifuni Lusiru alipongeza Mchakato mzima wa Uchaguzi namna ulivyoenda na kusema kuwa ulikua huru na wa haki. Imetolewa na; Kitengo Cha Mawasiliano na Masoko Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere 30.05.2026 Read more >
[ 2026-06-02 ]
Visitors Counter
Flag Counter
Collaboration

TCU Link

NACTE Link
NECTA Link
ZHELB Link
HELSB Link
MoEST Link
MoEZ Link
Social Networks
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter
Contact us
Hotline : +255 (22) 2820041/47
P.O.BOX : 9193 Dar es Salaam,TANZANIA
Email : rector@mnma.ac.tz
Location : Kivukoni Dar-es-salaam
W
E
L
C
O
M
E