PROF. MAPESA AMEMUAPISHA WAZIRI MKUU WA SERIKALI YA WANAFUNZI -MASO
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa Haruni Mapesa, Jana tarehe 9.06.2016 amemuapisha Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi, (MASO) Abubakar Rajab ambapo amemtaka Waziri Mkuu huyo kuwa daraja kati ya Uongozi wa Chuo, Rais wa Serikali ya Wanafunzi na wanafunzi wote huku akisisitiza umuhimu wa kutekeleza majukumu kwa staha. Mkuu huyo Taasisi, amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii na kufaulu vizuri masomo kwani ndiyo jukumu kuu lililowaleta chuoni. Aidha amewataka viongozi wa Wanafunzi kuunga mkono juhudi za uongozi wa Chuo kat ... ka kuhamasisha utunzaji wa mazingira, kulinda rasilimali za chuo. Kwa upande wake, Naibu Mkuu wa Chuo anayesimamia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa kitaaluma, Profesa Richard Kangalawe, amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii na kuzingatia taratibu za mitihani. Ameongeza kuwa ustawi wa wanafunzi unapaswa kupewa kipaumbele katika kipindi chote cha masomo chuoni, ili kuhakikisha wanahitimu wakiwa na Nidhamu, Maarifa na Ujuzi. Naye Naibu Mkuu wa Chuo anayesimamia Mipango, Fedha na Utawala, Profesa Evaristo Haulle amesisitiza kuwa ushirikiano wa dhati kati ya Uongozi wa Chuo na Serikali ya na Wanafunzj ni msingi katika kufanikisha malengo ya chuo na kuimarisha mshikamano wa kijamii. Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Masoko Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere 10.06.2026 Read more >
[ 2026-06-10 ]
Visitors Counter
Flag Counter
Collaboration

TCU Link

NACTE Link
NECTA Link
ZHELB Link
HELSB Link
MoEST Link
MoEZ Link
Social Networks
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter
Contact us
Hotline : +255 (22) 2820041/47
P.O.BOX : 9193 Dar es Salaam,TANZANIA
Email : rector@mnma.ac.tz
Location : Kivukoni Dar-es-salaam
W
E
L
C
O
M
E