|
|
|
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE CHA ADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Haruni Mapesa amewataka Watumishi kuhakikisha wanapima afya zao mara kwa mara, kujitoa katika kichangia damu pamoja na kuzingatia mazoezi ili kujiepusha na maradhi yasiyoambukiza kwani bila afya njema hakuna linaloweza kufanyika.
Prof. Mapesa amesema hayo wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja iliyofanyika siku ya Jumatatu inayohusu Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi na Magonjwa sugu yasiyoambukiza ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambapo amesema kuna magonjwa ambayo ...
lazima tujiepushe nayo ikiwemo Ukimwi, kusisitiza kuwa kila mmoja wetu anapaswa kukemea juu ya usambazaji wa virusi hivyo kwani vinaangamiza Taifa.
Mkuu huyo wa Taasisi amewataka Watumishi wa MNMA kujiepusha na kila aina ya vitendo vinavyoashiria rushwa au kuendana na rushwa na kuwa rushwa ni adui mkubwa wa Maendeleo katika Jamii, Taasisi na Taifa kwa ujumla.
Naye Naibu Mkuu wa Chuo anaesimamia, Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaaluma Prof. Richard Kangalawe amesema Afya ni mtaji hivyo ni vyema watumishi wakazingatia semina za namna hiyo kwa lengo la kujifunza na kuelimisha wengine.
Kwa upande wake Naibu Mkuu wa Chuo, Mipango, Fedha na Utawala Prof. Evaisto Haulle amesema lengo la Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi ni kukumbushana masuala ya ugonjwa huo na kuwa Elimu hiyo ni muhimu katika miasha ya kila siku ya Mwanadamu. Alisisitiza kuwa semina hiyo pia inamsaidia yule ambaye ana maambukizi kuwa na namna bora ya kuishi na maambukizi pasipo kuambukiza wengine.
Viongozi hao pia wamewataka Watumishi kushiriki vikao na semina mbalimbali ambazo uongozi wa Chuo unaziandaa kwa lengo la kujifunza na kupokea maelekezo yanayotolewa ili kuendeleza uwajibikaji ili kufikia malengo ya Taasissi.
Wataalamu wa ndani na nje ya Chuo wamehusika kutoa semina katika maeneo mbalimbali ikiwemo Mapambano dhidi ya Rushwa, Changamoto ya Afya ya Akili, Masuala ya jinsia, Uchangiaji wa damu, huduma ya Upimaji wa VVU na Unasihi, na kufanyika kwa mashindano ya michezo mbalimbali.
Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka huu ni: Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
24.06.2026
Read more >
[ 2026-06-25 ]
|
|
|
|