|
|
|
WAKUFUNZI WATAKIWA KUTUNGA MITIHANI YENYE UMAHIRI ILI KUZALISHA WAHITIMU WENYE WELEDI
Naibu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere anaesimamia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaaluma Prof. Richard Kangalawe amewataka wakufunzi kushiriki kikamilifu na Kuzingatia mafunzo yanayolenga kujifunza utungaji wa mitihani kwa wakufunzi huku akisisitiza kuwa mafunzo hayo yana maana kubwa pale ambapo watayazingatia na kuyatumia kikamilifu katika majukumu yao ya kila siku.
Prof. Kangalawe amesema hayo jana juni 23,2026 katika Kampasi ya Kivukoni jijini Dar es Salaam wakati akifungua warsha ya siku 2 na kubainisha kuwa kipimo cha k ...
tambua kwamba Mwanafunzi ameelewa ni kufaulu Mtihani ambao ametungiwa na Mkufunzi wake.
Prof. Kangalawe amesema kuwa Mafunzo hayo yataleta Mapinduzi chanya kwa kuongeza Maarifa mapya na Ujuzi wa Kitaaluma utakaowawezesha wakufunzi wa MNMA kwenda sambamba na Mabadiliko ya sasa ya sekta ya Elimu.
Kwa upande wake, Naibu Mkuu wa Chuo anayesimamia masuala ya Fedha, Utawala na Mipango Prof. Evaristo Haulle alieleza kuwa lengo kuu la mafunzo hayo ni kuboresha utendaji kazi wa Wakufunzi na kusisitiza kuwa Mafunzo hayo yana umuhimu hivyo ni lazima yatumike ipasavyo ili kufidia thamani ya fedha zinazotumika kuyagharamia.
Prof. Haulle amewataka Wakufunzi kuhakikisha wanawajibika kwa vitendo kwani hiyo ndiyo njia pekee itakayosaidia kuonesha taswira bora ya Chuo mbele ya jamii na wadau wa Elimu kwani uwekezaji unaofanyika katika kuwajengea uwezo watumishi unapaswa kuleta tija inayoonekana.
Akizungumza na Wakufunzi hao, Mkurugenzi wa Huduma za Usaidizi wa Kitaaluma Dkt. Atupakisye Kalinga ameelezea faida za mafunzo hayo ni kuwa kila Mkufunzi atakuwa na uwezo wa kutunga mtihani unaopima uelewa wa kile alichofundisha hatua itakayosaidia kuzalisha Wahitimu bora na kuinua ubora wa Elimu pamoja na kukuza utambuzi na utashi wa Mwanafunzi kwenye masomo yake.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
24.06.2026
Read more >
[ 2026-06-25 ]
|
|
|
|