WAHITIMU MAFUNZO YA UONGOZI NA MAADILI WATAKIWA KUWA WABUNIFU, KUJIAJIRI NA KUWA MABALOZI WAZURI WA MNMA
Wanafunzi waliohitimu kozi na Mafunzo ya Uongozi na Maadilikatika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyererewametakiwa kuendeela kujituma, kuwa wabunifu na kutumiamafunzo waliyoyapata kwa ajili ya kujiajiri pamoja nakukabiliana na changamoto mbalimbali baada ya kumalizamasomo ya Chuoni. Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkuu wa Chuo ambaye pia niNaibu Mkuu wa Chuo anesimamia taaluma, Utafiti na Ushauriwa Kitaalamu Prof. Richard kangalawe wakati akifungaMafunzo ya Uongozi na Maadili ambapo amesisitiza kuwaElimu waliyoipata Chuoni na mada walizofundish ... a ikiwemomasuala ya Uongozi na Maadili, Mapambano dhidi ya Rushwa, Ajira na Uwekezaji pamoja na usimamizi wa fedha ziendeleekubakia katika maisha yao ya kila siku na sio kuishia kwenyeMadaftari. Kwa upande wake, Naibu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha naUtawala, Prof. Evaristo Haulle amewakumbusha WanafunziWahitimu kuwa Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyererekitabakia kuwa alama katika maisha yao kupitia Elimu,Maadili, Uzalendo na kuwa wanachotakiwa ni kuendeleza yotewaliyojifunza. Prof. Haulle amewataka Wahitimu hao kuendeela kuwamabalozi wazuri wa kukitangaza Chuo katika mtazamo chanyakatika jamii pamoja na kufuatilia tovuti ya Chuo kupitia anuaniya www.mnma.ac.tz, kurasa za Mitandao ya kijamii ikiwemoInstagram mnmatheofficial, X maarufu twitterMNMA_official ili kupata taarifa sahihi na matangazombalimbali yayohusu Taasisi. Naye Mtiva wa Kitivo cha Uongozi na Maadili Dkt. Adili Zella amewapongeza kwa kushiriki kikamilifua mafunzo hayomuhimu ambayo yamelenga kuwajengea uwezo katika Nyanja mbalimbali za kimaisha ikiwemo Uongozi na Maadili, kujiepusha na rushwa, kujituma kwa bidii na kuhakikishawaakuwa vijana wenye Maadili mema. Mafunzo hayo ya siku tatu ya Uongozi na Maadili yamehusishaWanafunzi Wahitimu zaidi ya 3,000 ambayo yametolewakuanzia Julai 27 hadi Julai 29, 2026 katika Kampasi yaKivukoni Jijini Dar es salaam. Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Masoko Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere 30.07.2026 Read more >
[ 2026-08-10 ]
Visitors Counter
Flag Counter
Collaboration

TCU Link

NACTE Link
NECTA Link
ZHELB Link
HELSB Link
MoEST Link
MoEZ Link
Social Networks
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter
Contact us
Hotline : +255 (22) 2820041/47
P.O.BOX : 9193 Dar es Salaam,TANZANIA
Email : rector@mnma.ac.tz
Location : Kivukoni Dar-es-salaam
W
E
L
C
O
M
E