CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE CHAPONGEZWA KUENZI WAASISI WA TAIFA.
Naibu spika wa Baraza la Wawakikishi Zanzibar Mhe.Mgeni Hassan Juma amekipongeza Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa maono ya kujenga jamii imara yenye Uzalendo, Amani na Umoja wa kitaifa na kuhakikisha vijana wanafahamu historia ya nchi yao. Mhe.Mgeni ameyasema hayo jana tarehe 3.04.2025 wakati wa kongamano la saba la kumbukumbu ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume Rais wa Kwanza na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi - Zanzibar lililofanyika katika chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Karume Zanzibar. Amesema Chuo kim ... onesha njia nzuri katika kuwaenzi waasisi wa Taifa kwa kuwakusanya watu wa kada mbalimbali na rika tofauti kwenye makongamano ambayo yamekuwa yakifanyika katika Chuo hicho, hivyo ameziasa Taasisi nyingine l kuiga mfano huo na kuhakikisha vijana wanafahamu historia ya Taifa lao. Mhe.Mgeni amesema ili kumuenzi vizuri Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume jamii inapaswa kuzingatia mambo ambayo Marehemu Mzee Karume aliyasimamia ikiwa ni pamoja na Umoja wa kitaifa, Haki, Misingi bora ya kiuchumi,upendo na Amani. Awali akimkaribisha mgeni rasmi Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Mhe. Stephen Wasira amesema historia ya Zanzibar kamwe haiwezi kuandikwa bila kumtaja Muasisi wa Taifa hilo, Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume au kuyataja aliyoyafanya kwa ajili ya Taifa. Mhe. Wasira amesema, Marehenu Mzee Karume alileta Usawa katika Elimu na kuhakikisha huduma za Afya zinatolewa bure kwa wote huku akipiga vita dhuluma na kutetea haki za wazanzibari. Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa Haruni Mapesa amesema kuwa chuo kimekuwa na tamaduni ya kuwaenzi Waasisi wa Taifa na kuendeleza falsafa na Maono ya kuanzishwa kwa Chuo hicho ambazo ni Maadili, Uzalendo Uadilifu, Amani, na Maridhiano. Pamoja na hayo Prof. Mapesa amesema kuwa katika kila kozi inayotolewa Chuoni hapo ni lazima kila mwanachuo asome somo la Maadili ,Uzalendo na Utawala bora ili kuhakikisha vijana wa Taifa la Tanzania wanajua historia ya nchi yao. Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Masoko CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE 4.4.2025 Read more >
[ 2025-04-06 ]
Visitors Counter
Flag Counter
Collaboration

TCU Link

NACTE Link
NECTA Link
ZHELB Link
HELSB Link
MoEST Link
MoEZ Link
Social Networks
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter
Contact us
Hotline : +255 (22) 2820041/47
P.O.BOX : 9193 Dar es Salaam,TANZANIA
Email : rector@mnma.ac.tz
Location : Kivukoni Dar-es-salaam