|
|
WAZIRI MKUU MAJALIWA AWATAKA MADEREVA WA SERIKALI KUTUNZA SIRI ZA VIONGOZI NA KUFUATA SHERIA ZA BARABARANI.
Mhe.Kassimu Majaliwa amewataka Madereva wanaoendesha Magari ya Serikali kuhakikisha
wanakuwa na Weledi, Nidhamu na kuhakikisha wanakuwa nadhifu kimavazi muda wote wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku.
Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo jana tarehe 2.08.2025 wakati wa kongamano la Nne la Madereva wa Serikali wa Tanzania linalofanyika mkoani Dodoma, ambapo Madereva kumi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kutoka Kampasi zake tatu wanashiriki mafunzo hayo.
Waziri Mkuu Majaliwa amewataka Madereva hao kuhakikisha wanakagua gari mar ...
kwa mara ,kujaza kumbukumbu ya gari kwenye kitabu maalumu (Logbook) kabla na baada ya safari.
Pia amewataka Madereva kuhakikisha wanatunza siri za viongozi wao na kuwa wasiwe wanatoa taarifa za Viongozi wao pindi wanaposikia mazungumzo ndani ya gari.
Amewataka madereva Kujiepusha na kutumia namba za Magari ambazo siyo rasmi na kuacha kufunga vimulimuli kwenye magari kinyume na utaratibu.
Waziri Mkuu pia amewataka Madereva kufuata sheria na kuwa na nidhamu barabarani kwa kuheshimu alama za barabarani, kuacha kutumia vilevi, kutumia simu wakati wanapokuwa wanendesha gari.
Kauli mbiu ya kongamano hili ni ; Dereva wa Serikali epuka ajili, linda gari lako na watumiaji wengine wa barabara na shiriki uchaguzi Mkuu wa oktoba,2025.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
3.08.2025
Read more >
[ 2025-09-03 ]
|
|
|
|