|
|
|
WANAFUNZI MNMA WAPONGEZWA KUFANYA VIZURI KATIKA MICHEZO
Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Vyuo Vya Elimu ya Juu Tanzania- Shimivuta yamefungwa rasmi leo mkoani Tabora, huku Mashindano hayo yakitimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.
Akifunga Mashindano hayo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Tabora, Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora Dkt. John Pima ameyataka Makampuni mbalimbali kujitokeza na kufadhili Mashindano hayo, huku akiwataka Wakuu wa taasisi kutenga bajeti pamoja na kuruhusu washiriki kushiriki Mashindano hayo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. ...
Haruni Mapesa, Naibu Mkuu wa Chuo, Mipango,Fedha na Utawala Prof. Evaristo Haulle amewapongeza wanafunzi wa Chuo hicho kwa kupata ushindi wa Makombe mawili na cheti cha mchezaji bora kike wa mpira wa wavu.
Kombe moja ni kwa Mshindi wa kwanza katika mbio za magunia mita 100, kombe la pili ni mshindi wa tatu katika mpira wa wavu Wanawake
Prof. Haulle amesema ushindi huu umesaidia kukitangaza Chuo huku akiwataka Wanafunzi kuongeza juhudi katika kufanya mazoezi maana michezo ni furaha lakini pia ni ajira.
Viwanja vya michezo vilivyotumika kwa ajili ya michezo ya Shimivuta ni viwanja vilivyopo katika shule ya Wavulana Tabora na Shule ya Wasichana Tabora
Taasisi 16 zimeshiriki ambapo Kauli mbiu ya michezo kwa mwaka huu ni ; Miaka 50 ya Shimivuta, Michezo ni Afya.
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
22.12.2025
Read more >
[ 2025-12-28 ]
|
|
|
|