|
|
|
PROF. MAPESA AMSIMIKA MKURUGENZI MPYA KAMPASI YA KARUME - ZANZIBAR
Mkuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Haruni Mapesa amemsimika rasmi Dkt. Sifuni Lusiru kuwa Mkurugenzi mpya wa Kampasi ya Karume Zanzibar kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Januari 10, 2026 hadi 2028.
Katika kikao cha kumsimika na kumtambulisha Mkurugenzi mpya wa Watumishi wa Kampasi hiyo, Profesa Mapesa amewataka Watumishi wote wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere hususan watumishi wa Kampasi ya Karume Zanzibar kumpa ushirikiano wa dhati utakaofanikisha kutafsiri Falsafa na Maono ya Mkuu wa Chuo katika kuongoza kampas ...
hiyo.
Mkuu huyo wa Taasisi amemwelekeza Mkurugenzi huyo mpya na Watumishi wote kuongeza Kasi katika utendaji wa majukumu ili kuleta matokeo Chanya katika kufikia malengo ya Taasisi na taifa kwa ujumla.
Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi huyo mpya ameishukuru Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kumuona anafaa na kisha kumteua ili kuongoza nafasi hiyo, huku akiomba ushirikiano kutoka kwa watumishi wote wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Kwa upande wake Mkurugenzi aliyemaliza muda wake Dkt. Rose Mbwete amempongeza Dkt. Sifui kwa kuteuliwa kuwa Mkurugenzi mpya wa Kampasi ya karume ambapo amemsihi kuendelea kuwa imara, mvumilivu na kuhakikisha anakuwa karibu na Watumishi kwa lengo la kufanikisha malengo ya Chuo.
Imeandalilwa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
14/01/2026
Read more >
[ 2026-01-20 ]
|
|
|
|