-
Kutoa vifaa vya
masomo na programu za mafunzo katika sayansi ya jamii,
uongozi na elimu endelevu na Sayansi shirikishi;
-
-
Kushiriki
katika utafiti na maendeleo katika taaluma
zilizoainishwa katika aya ya (a) na kutathmini matokeo
yaliyopatikana kupitia programu za mafunzo ya Chuo
hicho;
-
-
Kutoa huduma za
ushauri kwa umma na sekta binafsi katika nyanja maalumu
kama ilivyoainishwa katika Sheria Namba 6 ya 2005;
-
-
Kudhamini,
kupanga, kuwezesha na kutoa vifaa vya mikutano,
makongamano, semina na warsha za majadiliano ya mambo
yanayohusu sayansi ya jamii, uongozi na elimu endelevu;
-
-
Kufanya
mitihani na kutunuku tunzo za Chuo kama ilivyoidhinishwa
na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi.
-
-
Kupanga
shughuli za uchapishaji na usambazaji wa jumla wa vifaa
vinavyozalishwa kutokana na kazi na shughuli za Chuo.
-
-
Kushiriki
katika shughuli za kuongeza kipato kwa ufanisi na kukuza
ujasiriamali.
-
-
Kuanzisha na
kukuza ushirikiano wa karibu na Vyuo Vikuu na taasisi
nyingine za elimu ya juu na kukuza ushirikiano wa
kimataifa na taasisi zinazofanana kimalengo na chuo.
-
-
Kufanya
shughuli na miamala yote kama ilivyopendekezwa na Bodi
ya Uongozi au suala muhimu kwa utekelezaji mzuri wa
majukumu ya Chuo.
-
-
Kufanya kazi
nyingine ambazo Waziri au Bodi ya Uongozi inaweza
kuelekeza kwa Chuo, au kama ilivyo kawaida au inayofaa
kwa maslahi ya Chuo au kazi nyingine zilizopo.