HUDUMA
ZA
MAKTABA
Maktaba
ndiyo
moyo wa
Kampasi
na ni
sehemu
muhimu
ya
dhamira
ya CKMN.
Dhamira
yake ni
kuhakikisha
kwa
wakati
wote
ujifunzaji
unafanyika
kwa njia
zilizo
bora
kuanzia
katika
ufundishaji,
utafiti,
ushauri
wa
kitaalamu
na
utumishi
wa umma.
Lengo
ni
kuhakikisha
kunakuwa
na
mazingira
mazuri
ya
kujifunzia
yenye
kulenga
kuchagiza
utafutaji
wa
maarifa
zaidi,
kukuza
ubunifu,
kukuza
fikra
kwa
utunduizi
na
ustadi
ulio
endelevu.
Maktaba
hutoa
huduma
ya
habari
kwa
watumiaji
wa
maktaba
wa ndani
na nje
ya
Kampasi.
Huduma
zinazotolewa
ni
pamoja
na
kuazima
vitabu
vya
maktaba
na
huduma
za
utoaji
wa
nyaraka.
.
USAJILI
WA
UANACHAMA
|
-
Wanafunzi wote waliosajiliwa na wanataaluma wa Chuo wanastahiki kutumia na kuazima vifaa (Vitabu, vitabu vya miongozo, n.k.) kutoka kwenye Maktaba.
-
Wafanyakazi wengine walioajiriwa na CKMN au wafanyikazi wa Kada nyingine pia wanaruhusiwa kutumia maktaba ingawa hawaruhusiwi kuazima vitabu isipokuwa kwa ruhusa maalumu kutoka kwa Mkuu wa Chuo au Mkuu wa Maktaba. Ikiwa ruhusa hiyo itaolewa basi, Mfanyakazi huyo atahitajika kuwasilisha kitambulisho chake.
-
Watumiaji wa nje: - Ambao si wanachuo au wafanyakazi wa Chuo hawawezi kutumia maktaba wala kuazima nyenzo au vitabu vyovyote kutoka Maktaba isipokuwa kwa ruhusa maalumu kutoka kwa Mkuu wa Chuo.
WATUMIAJI WA MAKTABA YA CKMN:
Watumiaji wa maktaba ya CKMN ni wanajumuiya Wa CKMN na watumiaji wengine walioidhinishwa kutoka nje ya CKMN wakiwamo watafiti kutoka ndani na nje ya Tanzania.
TARATIBU ZA UPATIKANAJI HUDUMA:
Upataji wa huduma za maktaba ya CKMN ni BURE (bila malipo) kwa sasa.
Watumiaji wote wa maktaba ya CKMN wanatakiwa kuzingatia Kanuni na taratibu zake.
|
KANUNI
ZA
MAKTABA
|
-
Maktaba itatumika kwa kujisomea na kuazima vitabu au nyenzo nyingine za taarifa kwa wananchuo na wafanyakazi wanataaluma.
-
Kwa sasa wafanyakazi wote wa CKMN walioajiriwa kutoka kundi la wafanyakazi ambao sio wanataaluma wanaweza kuruhusiwa kutumia huduma za maktaba ingawa hawaruhusiwi kuazima vitabu au nyenzo nyingine za taarifa kutoka maktaba
-
Watu ambao sio wanafunzi na wala si waajiriwa wa Chuo pamoja na watumiaji kutoka nje ya Chuo hawaruhusiwi kutumia huduma za maktaba. (Isipokuwa kwa idhini maalumu kutoka kwa Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma au Mkutubi Mkuu)
-
Hakuna waraka au nyaraka yoyote itakayotolewa au kupatiwa mtumiaji kutoka maktaba mpaka pale itakapokaguliwa na kuidhinishwa rasmi na wafanyakazi wa maktaba.
|
|