Utafiti na Ushauri
wa kitaalamu ni moja
ya Vitengo katika
Chuo ambapo kitengo
hiki kinashughulikia
huduma za Utafiti na
Ushauri wa kitaalamu
kwa jamii. Kitengo
kilianzishwa kwa
lengo la kuendesha
na kuratibu shughuli
za utafiti na
kuwezesha
kubadilishana
maarifa. Shughuli za
utafiti hufanywa kwa
njia ya kimfumo
inayolenga
kushirikisha Chuo na
wadau tofauti wa
utafiti kama
serikali, viwanda,
Asasi zisizo za
kiserikali, kampuni
za madini na mafuta
na kampuni za ujenzi
ambazo zinakusudia
kutumia tafiti
kusaidia shughuli
zao.
Shughuli za utafiti
hufanywa katika
vikundi vyenye
tajriba mbalimbali
kwa kushirikisha
idara mbalimbali
ambazo ni pamoja na
idara ya Sera ya
Umma, Masuala ya
Jinsia, Uhusiano wa
Kimataifa, Utawala
Bora, Uchumi na
Usimamizi wa
Rasilimali watu.
Idara hii ina Jarida
moja lililosajiliwa
kwa namba ya usajili
ISSN 1821 - 6989 na
iko kwenye mchakato
wa kuzindua Jarida
kuwa jarida
litakalopatikana la
mkondoni.
Tunayo raghba na
hamu ya kukuza
tafiti zetu kupitia
viungo (links)
mbalimbali kwa
kushirikiana na
wasomi wa kimataifa
ambao wana mawazo,
fikra na mitazamo
mipya anuwai.
MAELEZO YA KITENGO
CHA UTAFITI NA
USHAURI WA KITAALAMU
Chuo kimedhamiria
kutoa tafiti za hali
ya juu ili ziweze
kuleta athari kwa
jamii ya kitaifa na
ya kimataifa ili
kuchochea
upatikanaji wa fedha
za kuwafadhili
washiriki na
wanachuo
wanaotarajiwa
kufanya tafiti za
uzamili.
Kitengo cha Utafiti
na Ushauri wa
kitaaluma
kinahakikisha kuwa:
Tafiti zilizofanywa
zinakuwa bora zaidi
na zinazoweza
kutumiwa na wadau wa
utafiti katika
usimamizi,
utekelezaji na
tathmini ya mipango
yake.
1. Matokeo ya
utafiti hutumiwa
vizuri katika
kutatua na kujibu
shida.
2. Tafiti zote
hupitiwa na
kutathminiwa kufikia
viwango vya kidunia
na vya kimataifa.
3. Mada za utafiti
na maswali ni muhimu
na ziko katika
vipaumbele vya Chuo.
4. Kuhakikisha
zinatumika njia
tmbalimbali za
kitaaluma katika
tafiti zote ili
kupata matokeo bora
zaidi ya kisayansi.
5. Wanataaluma
kutoka fani
mbalimbali wanatumia
tafiti hizo
kuhakikisha wanatoa
huduma za Ushauri wa
kitaalamu kwa
taasisi za serikali
na binafsi na ndani
na nje ya nchi.
SHABAHA NA MALENGO
Kitengo cha Utafiti
na Ushauri wa
kitaalamu cha Chuo
kinahakikisha kuwa
matokeo ya tafiti
yanayotokana na
tafiti za wataalamu
wake yanatumiwa na
wadau wa utafiti
ikiwamo serikali,
viwanda, Asasi za
Kiraia na kampuni
mbalimbali kuhusu
mipango yao, uamuzi,
na sera ili
kuboresha shughuli
zao za kila siku
ambazo zinaweza
kuleta mabadiliko
makubwa nchini.
UPIMAJI WA SHUGHULI
ZA UTAFITI
Ili kuhakikisha
tafiti zake zinakuwa
bora, Chuo kupitia
kitengo cha utafiti
na ushauri wa
kitaalamu kina
kawaida kufanya
tathimini ya pamoja
kwa kufanya majopo
anuwai ya wataalamu
yenye lengo la
kutathmini matokeo
ya utafiti
uliofanywa na
wataalamu wa Chuo
yanafikiwa. Tathmini
huongozwa na mambo
yafuatayo, maudhui
yaliyoandikwa kwenye
mada, uhalisia wa
kazi yenyewe ya
utafiti, Mchango
maudhui ya Maarifa
ya utafiti huo,
uhusiano wake katika
taaluma, Umuhimu
kitaaluma kwa Watu
binafsi walioko
katika uwanja huo wa
Taaluma,
Uwasilishaji na
Ubora wake kwa jumla.
BODI YA UHARIRI
Chuo kina Bodi ya
Wahariri ya kukagua
masuala ya maadili
na kuhakikisha
viwango vya ubora
vinazingatiwa na
watafiti wakati wa
kufanya utafiti na
katika mchakato wa
uchapishaji pia.