
KONGAMANO LA KUMBUKIZI YA KUZALIWA MWALIMU JULIUS K. NYERERE
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko akisikiliza maelezo kuhusu majarida na machapisho mbalimbali wakati wa kongamano la kumbukizi ya kuzaliwa Muasisi wa Taifa Mwalimu JK, anayetoa Maelezo ni Mkufunzi Msaidizi huduma za Maktaba Kanyinyi Kimolo.
KONGAMANO LA KUMBUKIZI YA KUZALIWA MWALIMU JULIUS K. NYERERE
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Mwenyekiti wa bodi ya Chuo Mhe. Stephen Wasira akimkabidhi zawadi ya tuzo Mgeni rasmi Mhe. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Biteko wakati wa Kongamano la kumbukizi ya kuzaliwa Baba wa Taifa Mwalimu JK. Nyerere lililofanyika Chuoni hapo.
SIKU YA WANAWAKE 2025
Baadhi ya Wanawake wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani ambapo kwa mkoa wa Dar es salaam yalifanyika katika viwanja vya Leaders Club Wikayani kinondoni.
SHIMIVUTA 2024
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Haruni Mapesa akiwa ameshika kombe la ushindi, baada ya wanafunzi wa Chuo hicho walioshiriki mashindano ya SHIMIVUTA kuibuka washindi katika mchezo wa wavu. Mashindano hayo yalifanyika mwaka jana katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
ZIARA YA KANSELA WA UBALOZI WA CHINA
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Haruni Mapesa aliyesimama katikati akiwa katika picha ya pamoja na Kansela wa Ubalozi wa China nchini Tanzania Xu Sujiang kutoka idara ya kimataifa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomonisti cha China(IDCPC), ambaye amesimama upande wa kushoto.
MAHAFALI YA TISA KAMPASI YA KARUME ZANZIBAR
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo, Mzee Stephen Wasira na Mkuu wa Chuo Prof. Haruni Mapesa wakiongoza Maandamano ya Wajumbe wa Bodi, Wakurugenzi, Wativa na Wahitimu wakati wa Mahafali ya 2 Kampasi ya Karume, eneo la Bububu Visiwani, Zanzibar ambapo Wahitimu zaidi ya 1200 wamehitimu kozi mbalimbali.
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE NA WIZARA YA UTAMADUNI
Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere leo wameshiriki katika hafla ya pamoja ya kutia Saini hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika Kutambua,kuhifadhi,Kulinda,kuendeleza na kutangaza urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika.
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ELIMU, UTAMADUNI NA MICHEZO
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Mzee Stephen Wasira akiwa na kamati ya kudumu ya Bunge Elimu, Utamaduni na Michezo ilipotembelea Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kampasi ya Karume tarehe 26.8.2023 kukagua ujenzi wa mradi wa Hostel za wanafunzi za Chuo.
UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI - KAMPASI YA PEMBA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la majengo ya Chuo, Kampasi ya Pemba.
UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI - KAMPASI YA PEMBA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi akiweka jiwe la msingi ujenzi wa Kampasi ya Pemba.