Chuo cha Kumbukumbu
ya Mwalimu Nyerere (CKMN)
ni taasisi ya elimu
ya juu iliyotokana
na Chuo cha Kivukoni
kilichoanzishwa
mnamo tarehe 29
Julai, 1961. Chuo
kina historia ya
kuwa taasisi pekee
ambayo imehifadhi
kumbukumbu muhimu za
kuwajengea uwezo
viongozi wa umma
katika fani ya
uongozi na maadili,
hususan wakati wa
kipindi cha mfumo wa
uongozi na utawala
wa chama kimoja.
Shabaha ya CKMN ni
kuhakikisha kwa
wakati wote
ujifunzaji
unafanyika kwa njia
zilizo bora kuanzia
katika ufundishaji,
utafiti, ushauri wa
kitaalamu na
utumishi wa umma.
Lengo ni kuhakikisha
kunakuwa na
mazingira mazuri ya
kujifunzia yenye
kulenga kuchagiza
utafutaji wa maarifa
zaidi, kukuza
ubunifu, kukuza
fikra kwa utunduizi
na ustadi ulio
endelevu.
CKMN kina maktaba
nzuri. Watumiaji
wote wa Maktaba ya
CKMN wanapaswa
kuzingatia sheria na
kanuni za makatba.
Shughuli za Maktaba
ya CKMN zinalenga
kurahisisha shughuli
za ufundishaji na
utafiti wa Chuo
kupitia utoaji wa
vitabu, majarida,
magazeti na vifaa
vingine vya kusoma
kwa wahadhiri,
wafanyakazi wa
utawala, wanachuo na
watafiti wengine.
Wanafunzi wana uhuru
kamili wa kuabudu,
ila uhuru haupaswi
kuchupa mipaka na
kukera au kuzuia
uhuru wa wengine
kufurahia kwa namna
yoyote ile. Aidha,
uhuru huo haupaswi
kuzuia shughuli
nyingine za CKMN
kuendelea. Huduma za
kiibada kwa
madhehebu yote
makubwa hupatikana
kwa umbali wa
kutembea tu kwa mguu
kutoka CKMN.
CKMN kinahimiza
wanafunzi kushiriki
katika shughuli
mbalimbali za
michezo na burudani.
Huduma za michezo
zinazopatikana
katika Chuo ni
pamoja na uwanja wa
mpira wa miguu,
uwanja wa mpira wa
mikono, uwanja wa
mpira wa kikapu na
wa mpira wa wavu.
Wanafunzi wanapata
huduma za matibabu
katika zahanati ya
CKMN, ambayo
inaongozwa na
mtaalamu wa matibabu.
Kwa maradhi au shida
zote kubwa za kiafya
zinazohitaji
uangalifu maalumu
hupelekwa katika
hospitali
zinazohusika.
Kwa taarifa zaidi za
Chuo peruzi zaidi
tovuti hii ili
kupata uelewa mzuri
zaidi kuhusu CKMN.
Ni imani yetu kuwa
tovuti hii
itakunufaisha zaidi
na itakuwa msaada
kwako.
Asanteni sana na
karibuni Chuo cha
Kumbukumbu ya
Mwalimu Nyerere
Prof
Shadrack S.
Mwakalila
Mkuu wa Chuo